Miongoni mwa makosa yanayofanyika mtandaoni ni hili lijulikanalo kama “Phishing” ambapo kosa hili limekuwa likidumu na kukua kwa kasi sana katika nchi mbali mbali.
Nchi mbali mbali zimechukulia uhalifu huu kuwa ni hatari kwani unaweza kuwa na madhara makubwa kwa mtendewa ikiwa ni pamoja na kupelekea kumfilisi mtu, kupata taarifa za watu kinyume na sheria au makubaliano na hata wakati mwingine kupelekea kuleta madhara mengine kama kutumika kuhatarisha mifumo mbali mbali.
Kwa kuzingatia hili nchi mbalimbali zimekuwa na sheria kali dhidi ya uhalifu huu , huku nchi za afrika kupitia umoja wa wataalam wa maswala ya usalama mtandaoni wamekubalina kuanzisha kamati yenye watu maalaum itakayoangazia macho uhalifu huu na kutoa taarifa huku hatua zikichukuliwa.
Makampuni ya Ati-vurus nayo yametoa uzito kwenye hili na kuhakikisha wanaunda nyezo madhubuti za utambuzi wa aina hii ya uhalifu na mara kwa mara wakiwasilisha ripoti zao.
Changamoto bado zipo kutokana na upungufu wa uelewa kwa wananchi mbali mbali juu ya uhalifu huu inayo sababisha waathirika kueendelea kuwa wengi kila kukicha.
Uchunguzi umeonyesha mara nyingi panapokuwa na jambo linalo fuatiliwa na wengi, wahalifu nao hujipenyeza hapo na kuanza kusambaza aina hii ya uhalifu.
Kwa upande wa Tanzania, Serikali imekuwa ikizungumza mara nyingi na kutoa tahadhari mbalimbali juu ya uharifu wa kimtandao.
Ni vizuri tukakumbushana kuwa Tanzania imesha kamilisha rasimu ya sheria za mitandao ambazo zitatoa fursa kwa wahalifu kushughulikiwa ipasavyo na hivi karibuni TCRA nayo ilizungumzia mpango wake wa kushughulikia watumiaji vibaya wa mitandao. Hili likiwa linafuatia kampeni yao ya Futa delete kabisa.
Wakati hili linajiri, kumekuwepoa na wimbi la wahalifu wa uhalifu huu wa "Phishing" ambao hudukua na kuchukua akauti za mitandao za watu na kuanza kusambaza taarifa zitakazo wawezesha kupata taarifa za wengine na mara nyingine wanatengeneza akaunti feki za mitandao wakitumia majina ya watu maarufu na kuanza kuzitumia vibaya.
Waharifu hao wamekuwa wakitumia majina ya watu mashuhuri na kutumia watu ujumbe wakiwataka wabonyeze link ili kujiunga na huduma kama Vikoba, Pia wamekua wakituma ujumbe wakiwataka watu wafungue tovuti n.k
TAHADHARI: Kila mmoja anapaswa kuwa makini na unapo hisi ya kuwa unaweza ukawa muathirika wa uhalifu wa huu kimtandao basi badilisha neno la siri na siku zote jiepushe kujibu au kufuata maelekezo yatakayo kutaka ufanye kitu Fulani.
0 Comments