Header Ads Widget

HIZI NDIO SABABU KUMI NA NANE ( 18 ) KWA NINI UNATAKIWA KUPUNGUZA UZITO.








Unene ni tatizo linalo wakabili watu wengi duniani. Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kitaalamu, unene una madhara makubwa kuliko inavyo dhaniwa.
Hizi ni sababu 18 kwa nini unatakiwa kupunguza unene.


1. Unene unaongeza kiwango cha mafuta mwilini, ambayo huongeza uwezekano wa kupata kansa.


2. Unene unaongeza mafuta mwilini, ambayo hufanya matibabu ya kansa kuwa magumu zaidi.


3. Unene huongeza mafuta mwilini ambayo hushinikiza na kuubana moyo.


4. Mtu mnene huwa mvivu kufanya mazoezi, suala ambalo humuongezea zaidi unene.


5. Mafuta mengi mwilini yana madhara kwa ubongo.


6. Unene huongeza uzito katika mifupa na viunga vya mifupa ( bone joints )


7. Unene husababisha kibofu cha mkojo kibanwe suala linalo sababisha matatizo mbalimbali ya mkojo.


8. Unene hupunguza uwezo wa kujamiiana wa mtu.


9. Unene hupunguza uwezo wa kuzaa na hata kusababisha utasa na ugumba.


10. Unene husababisha kibofu cha mkojo kibanwe, suala linalo sababisha matatizo mbalimbali ya mkojo.


11. Unene huweza kuufanya mwili upatwe kwa wepesi na magonjwa mbalimbali kama vile kisukari na presha.


12. Watu wanene wanapofika hospitalini, upimaji wao pia huwa wa matatizo.


13. Unene husababisha ujauzito kuwa wenye matatizo mengi.


14. Unene huathiri pia afya ya motto mchanga anaye zaliwa.


15. Unene hufanya matibabu ya pumu ( asthma ) yawe magumu.


16. Unene hupelekea mtu asilale vizuri na wakati mwingine mtu mnene anapolala hubanwa na pumzi suala linalo mfanya aamke mara kwa mara.


17. Unene humfanya mtu ashindwe kuwajibika vizuri kazini na hata kuathiri utendaji kazi wake.


18. Unene hufanya matumizi ya fedha kuwa makubwa unapokumbwa na magonjwa yasababishwayo na unene.

Post a Comment

0 Comments