Mwanamuziki mkongwe na Gwiji la muziki wa dansi nchini Tanzania, Maalim Muhidin Gurumo, (pichani enzi za uhai wake) aliyefariki dunia jana jioni majira ya saa 9 alasiri katika hospitali ya Taifa Muhimbili, anatarajia kuzikwa leo Adhuhuri huko kijijini kwao Masaki Kisarawe.
Kwa mujibu wa makamu wa Rais wa Chama cha Muziki Tanzania anayefahamika kwa jina la Brighton, Marehemu mzee Gurumo alipelekwa hospitali ya Muhimbili juzi alfajiri baada ya hali yake kubadilika ghafla, na kulazwa katika wodi ya Kibasila kwa ajili ya matibabu.
Aidha taarifa kutoka kwa meneja wake zinasema kuwa Marehemu mzee Gurumo alikuwa akisumbuliwa na taizo la mapafu kujaa maji.
0 Comments