Header Ads Widget

HAYA NDIYO MATOKEO YA JANA YA LIGI YA MABINGWA ULAYA REAL MADRID YATANGULIA FAINALI, YAICHAPA BAYERN MUNICH 4-0 NYUMBANI .



Timu ya soka ya Real Madrid toka Hispania baada ya kusubiri kwa miaka 12 hatimaye usiku wa kuamkia leo imekata tiketi ya kucheza fainali ya ligi ya mabingwa Barani Ulaya baada ya kuifunga bila huruma Bayern Munich mabao 4-0 katika mchezo wa pili wa nusu fainali ya ligi ya mabingwa Ulaya, mchezo uliochezwa katika uwanja wa Allianz Arena usiku wa kuamkia leo.

Mabao toka kwa Sergio Ramos aliyeifungia Madrid mabao mawili makali kwa kichwa kunako dakika za 16 na 20, na baadaye mabao mengine mawili toka kwa mshambuliaji aliye katika kiwango cha hali ya juu Duniani kwa sasa, Cristiano Ronaldo katika dakika za 34 na 88, yalitosha kabisa kuwanyamazisha mashabiki wa Bayern Munich waliokuwa wakishangilia kama nyuki baada ya kushuhudia timu yao ikilala nyumbani tena kwa aibu kubwa.

Bayern Munich waliokuwa mabingwa watetezi, sasa wameuvua ubingwa huo na kuuacha mikononi mwa ama Real Madrid, au mshindi wa mchezo wa leo kati ya Chelsea dhidi ya Atletico Madrid, ambapo mshindi wa mchezo huo atakutana na Real Madrid katika mchezo wa fainali utakaochezwa Lisbon, Ureno May 24 mwaka huu.

Franck Ribery akimpiga kibao Carvajal, kitendo hicho hakikuonekana na mwamuzi wa mchezo huo Pedro Proenca toka Ureno.

Duh!! Nasikia kama shingo inaanza kuuma kwa mbaaaali.

Kocha wa Bayern, Pep Guardiola akishuhudia timu yake ilipokuwa inatandikwa bao moja baada ya jingine. Kwa ushindi huo wa mabao 4-0, Real imeitoa Bayern kwa jumla ya mabao 5-0, kwani katika mchezo wa kwanza, Madrid ilishinda kwa bao 1-0.

Post a Comment

0 Comments