
Cristiano Ronaldo amevunja rekodi iliyokuwa ikishikiliwa na Lionel Messi kwa kufunga magoli mengi katika Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya kwa msimu mmoja, wakati akiiongoza jana Real Madrid kuitoa katika michuano hiyo Bayern Munich na kutinga fainali za ligi hiyo.
Mchezaji huyo Mreno alifunga goli la 15 na la 16 katika ligi hiyo katika msimu huu wakati Real ikiidhalilisha Bayern kwa kuipa kipigo cha mabao 4-0 kwenye dimba la Allianz Arena, na kufanya matokeo ya jumla kuwa 5-0.
Mshambuliaji huyo wa zamani wa Manchester United kwa sasa ameshafunga magoli 67 katika michezo yote ya Ligi hiyo aliyowahi kucheza katika misimu yote akifungana na Lionel Messi.
CREDIT:RWEYUNGA BLOG
0 Comments