Alli kibwita mjukuu afariki huko mbagala kwa kupigwa risasi na majambazi usiku wa saa tatu jana ya tarehe 24.
Kijana huyo alikuwa anafanya kazi ya kuuza duka la sim na vocha maeneo ya mbagala,na huko ndiko kifo chake kilipomkuta.Aliyenipa taarifa hizo ni mmoja wa rafiki na ndugu wa marehemu ambaye wametokea sehemu moja inayojulikana kama kwamakocho.kwamakocho ni kjiji ambacho ametokea huyo marehemu alli kibwita.Aliyenipa taarifa hizi ni bwa HAMISI ABDALLAH MWELANGI.Alisema kwamba marehemu aliingiliwa na majambazi usiku sehemu ambayo alikuwa anafanya kazi ya kuuza vocha na simu huko mbagala na kupigwa bastola na hao majambazi kisha wakapola fedha na kuondoka. kwa bahati mbaya picha za tukio hazikupigwa tutokana na mtu aliyenipa taarifa alikuwa mbali na tukio.Maiti itasafirishwa leo kwenda katika kijiji cha KWAMAKOCHO Kwa ajili na maandalizi ya kuzika.ALLI KIBWITA MJUKUU Enzi za uhai wake. Mbele yako nyuma yetu sote tupo kwenye foleni.
Upunzike kwa amani KIBWITA MJUKUU.
0 Comments