Header Ads Widget

OMAR MOHAMED HUSSEIN KUTOKA MISRI AIBUKA MSHINDI WA KWANZA KATIKA MASHINDANO YA QUR'AN TUKUFU AFRICA

Mshindi wa kwanza mashindano ya quran tukufu afrika chini ya alhikma foundation

Picha ya Omar Mohamed Hussein Mshindi wa kwanza
Kijana wa misri mwenye umri wa miaka 22 aibuka mshindi katika mashindano ya kuhifadhi qur'an tukufu

Hatimaye leo ndio ilikuwa siku yenyewe ya mashindano ya kuhifadhi qur;an tukufu africa mashindano ambayo yanaendeshwa na taasisi ya Al hikma foundation chini ya Shekh Nurdeen Kishiki,

Leo Tarehe 09/04/2023 ndio ilikuwa siku ya mashindano haya na yalihudhudhuliwa na washiriki kutoka sehemu mbalimbali katika bala la afrika, Lakini hata hivyo kulikuwa na wageni watatu waalikwa katika mashindano hayo kutokea mabala tofauti tofauti ambayo ni, Bala la Asia nchi ya Saudia Rabia, Bala la Ulaya mshiriki kutokea nchi ya Wingereza na Bala la America Mshiriki kutoka Marekani

Nurdeen Kishk mwanzilishi wa mashindano

Mashindano haya yalikuwa mazuri sana yakihudhuriwa na mgeni rasmi Mheshimiwa Raisi wa Tanzania Visiwani Zanzibar Dr, Hussein Ally Mwinyi, Lakini pia Mufti wa Tanzania, Raisi Mstaafu wa awamu ya pili Mheshimiwa Ally Hassan Mwinyi, Shekh mkuu wa Dar es salaam Walidi Omary Kawambwa na wengine wengi waliohudhuria shughuli hii pamoja na kuwa na hali ya hewa ya mvua lakini mwitikio ulikuwa mkubwa

Mwisho mshindi akapatikana baada ya washiriki wote kusoma kwa kiwango kizuri kwa uwezo wake lakini siku zote mshindi lazima apatikane na alieshinda nafasi ya kwanza kwa usomaji bora ni Kijana Kutoka nchini Misri jina lake ni Omar Mohamed Hussein ambaye ndie aliejinyakulia kitita cha shilingi milini 23 za kitanzania huku nafasi ya tatu na nne zikienda kwa Kenya na Tanzania.

Tazama video akisoma kwa madaha mshindi huyo


Post a Comment

0 Comments