KWENYE ulimwengu wa mapenzi, hakuna kitu kibaya kama kusalitiwa na mpenzi wako tena unayempenda kwa dhati. Ni jambo linalouma sana kiasi cha kuwafanya baadhi ya watu kuchukua uamuzi wa kujiua kwa kunywa sumu na wengine kuchanganyikiwa.
Lakini mara nyingi sana wengi wanapenda kujua sababu zinazowafanya wepenzi wao wawasaliti ili waweze kuchukua hatua za kuhakikisha hayawakuti hayo. Leo kupitia ukurasa huu nimeona nikupe baadhi ya sababu ambazo huwafanya watu walio kwenye uhusiano kusaliti.
Sababu za Wanaume walio wengi wameingia kwenye mapenzi na wanawake wasioendana nao.
Hapa namaanisha kwamba wapo ambao anakutana na mwanamke, anaingia naye kwenye uhusiano kisha baada ya siku chache anagundua mtu huyo hakuwa mtu sahihi kwake. Matokeo yake sasa anashawishika kutoka nje ya uhusiano wake.
1. Ucheshi wa mwanamke
Wanaume walio wengi hawapendi wanawake watulivu. Hapa siongelei wanawake micharuko, naomba nieleweke vizuri. Wanaume hasa vijana wa sasa wanapenda wanawake ambao wapo kiuchangamfu zaidi, yaani amechangamka kwenye ubunifu wa mambo, utundu wa chumbani na hata ushapu kwenye mambo ya kidunia yanayoendelea.Asikudanganye mtu kuwa siku hizi wanaume eti wanapenda mwanamke ambaye ni wa kijijini, anayeanza naye moja kwenye kumfundisha. Aisee utashangaa mwenzako anakuacha ndani kisha anakwenda kwa mwanamke mwingine ambaye yupo tofauti na wewe.
2. Tendo la ndoa
Usije kujidanganywa kuwa eti kwa sababu uko poa kwenye mambo yetu ya sita kwa sita basi huwezi kusalitiwa, lahasha! Kumbuka kuwa tendo hilohilo linaweza kununuliwa akafanya yake na akamaliza lakini jiulize wale wanaosaliti halafu wanahamia moja kwa moja kwa wanawake inakuwaje? Kule hafuati tendo, kuna kitu cha ziada atakuwa anakifuata.
3. Mapishi na usafi
Kama wewe mwanamke hujui kuufanyia usafi mwili wako na hata mazingira ya nyumbani kwako, jua moja kwa moja mumeo atakusaliti na kwako atarudi kulala tu ilimradi kutimiza ndoa.Pia kuna suala la mapishi, kama wewe mwanamke hujui kumpikia mumeo chakula kizuri na kukibadili kila siku utasalitiwa tu. Wanaume ni watu wa kukinai mara moja unatakiwa kuwa mbunifu kwenye kila kitu.
4. Kuboreka
Hapa ndiYo nasisitiza lile suala la mwanamke kuwa mcheshi kwa mumewe, mfano kumtania mume, kuwa na furaha uwapo naye wakati wote. Wanaume ni wepesi kuboreka, kama atakuja nyumbani na kukukuta kwenye hali ya kila siku, mara ooh! Naumwa.Mara ooh! Jirani kanifanyia hivi, yaani lawama… lawama… mpaka usiku unaisha mnalala, mume ataboreka na kuhamia kwingine. Akina mama wengi wanapenda sana lawama, hawajui kuwa wanaume mambo hayo wakati mwingine hawayapendi.
Kama una lawama zako hebu subiri basi siku za wikiendi mkiwa mmetulia hasa mida ya chai ndiyo umpe lawama zote lakini siyo kila akirudi nyumbani.
Vijana wanakwambia unamkata ‘stimu’, kama alikuwa na hamu ya kitu kutoka kwako akikukuta uko kwenye mudi za lawama na visirani, anaishia hapo.
Kwa upande wa mwanamke Nao huwa na sababu za kusaliti lakini hapa nitaziongelea sababu kuu mbili ambazo mwanaume ukiziibua, mwanamke ni rahisi sana kuhamisha hisia na kuzipeleka kwingine.
0 Comments