Mwalimu mmoja ameuawa na watu wawili kujeruhiwa vibaya katika shambulio la kisu katika shule moja nchini Ufaransa, maafisa wanasema.
Waziri wa Mambo ya Ndani Gérald Darmanin alisema shambulio hilo lilitokea katika shule ya upili ya Gambetta katika mji wa kaskazini wa Arras.
Maafisa wa eneo hilo wanasema mshambuliaji huyo amekamatwa.
Mshambulizi huyo anaaminika kuwa na umri wa miaka 20.
Idhaa ya Ufaransa ya
BFMTV imeripoti kuwa ndugu wa mshambuliaji huyo pia amekamatwa na polisi.
Idhaa hiyo ilisema mtu aliyeuawa ni mwalimu wa lugha ya Kifaransa, huku mwalimu wa michezo pia akichomwa kisu na kujeruhiwa.
Vyombo vya habari vya eneo hilo vimeripoti kwamba mshambuliaji huyo alikuwa mwanafunzi wa zamani katika shule hiyo.
Polisi wanasema hali sasa imedhibitiwa.
Rais wa Ufaransa Emmanuel Macron atatembelea shule hiyo baadaye Ijumaa na kutoa pole kwa tukio hilo.
0 Comments