Header Ads Widget

SGA Security Yashinda Tuzo Ya Kampuni Bora Ya Ulinzi Afrika

SGA Security Yashinda Tuzo Ya Kampuni Bora Ya Ulinzi Afrika
Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya ulinzi ya SGA Tanzania, Bw Eric Sambu akionesha tuzo iliyokabidhiwa kampuni hiyo.

Kampuni ya ulinzi ya SGA Security imetangazwa mshindi wa jumla kati ya makampuni ya ulinzi Afrika katika tuzo za kampuni bora Afrika yaani Africa Company of the Year Awards 2023 zilizofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

SGA ilikuwa miongoni mwa makampuni mengine ya ulinzi yaliyochaguliwa kugombea tuzo hiyo baada ya mchujo mkali uliofanywa na wataalamu kutoka kwenye kampuni ya ukaguzi ya kimataifa.

Kwa mujibu wa waandaaji wa tuzo hizo kupitia jaji wao mkuu, Bw. Tom Onguru, washindani walishindanishwa katika vipengele saba ikiwemo uongozi, masoko, ,namna ya kuhudumia wateja, rasilimali watu, uzimamizi wa ubora, uzimamizi wa fedha na usimamizi wa masuala ya ICT na elimu. Washindani walitakiwa kuonesha vitibitisho kuwa wamefikia viwango vilivyowekwa na waandaaji.SGA Security Yashinda Tuzo Ya Kampuni Bora Ya Ulinzi AfrikaMkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SGA Tanzania, Bw Eric Sambu (kulia) akionesha tuzo iliyokabidhiwa kampuni hiyo baada ya kutangazwa kampuni bora ya ulinzi ya mwaka katika tuzo za kampuni bora Africa – Africa Company of the Year Award (ACOYA 2023) zilizofanyika Jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.

Akizungumza baada ya kupokea tuzo hiyo, Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni ya SGA Tanzania Bw. Eric Sambu alisema kampuni hiyo imepitia wakati mgumu hasa baada ya ongezeko la ghafla kwa kimo cha chini cha mshahara kwa asilimia 48 jambo ambalo lilifanya wateja wengi washindwe kumudu gharama za ulinzi , lakini kwa sasa hali imetengamaa.

Alisema kampuni hiyo inajiandaa kuadhimisha miaka 40 ya kutoa huduma nchini Tanzania na kuongeza kuwa SGA ndio ilikuwa kampuni ya kwanza ya ulinzi ya binafsi kusajiliwa Tanzania huku ikijulikana kama Group 4 Security (T) Ltd mwaka wa 1983. Kampuni hiyo, kwa mujibu wa Bw. Sambu, imeleta mabadiliko makubwa katika sekta ya ulinzi tangu muda huo na imeajiri zaidi wa watanzania 5000 ambao ni sehemu ya wafanyakazi 18,000 katika ukanda huu.

“Tuzo hii ni kwa ajili ya wafanyakazi wetu ambao mara zote huhakikisha wateja wetu wanapata huduma bora na hili linathibitisha na imani ya wateja katika huduma zetu. Hii inatupa moyo wa kufanya bidii zaidi ili tuwape huduma bora inayoendana na fedha wanazolipa,” alisema.

Alipongeza pia askari wa kampuni hiyo kwa ubora wao ambao unaifanya SGA iwe juu ya makampuni mengine. “Kuna ziadi ya makampuni 2000 ya ulinzi nchini Tanzania lakini kinachotutofautisha ni jinsi tunatoa huduma zetu. Tunawapa kipa umbele wafanyakazi wetu ili waendelee kufanya kazi kwa weledi na hata kuzidi matarajio ya wateja wetu,” alisema.

Kwa upande wake, Meneja Masoko wa SGA, Faustina Shoo alisema wamefarajika kupokea tuzo hiyo hasa baada ya kupitia kipindi kigumu kilichosababishwa na janga kubwa la UVIKO 19 na pia ongezeko la ghafla la kimo cha chini cha mshahara. “Sisi SGA tunazingatia sana mahitaji ya mteja. Licha ya changamoto zote tulizopitia, tumebaki imara kwa sababu ya umoja tuliojenga. Tunawashukuru sana wateja wetu na watanzania kwa ujumla kwa kutuunga mkono,” alisema.

SGA Security inatoa huduma mbalimbali kama vile ulinzi, alarm, usafirishaji wa fedha, ulinzi wa kielektronia, usafirishaji wa vifurushi na huduma nyinginezo. Kampuni hiyo ndio kampuni pekee ya ulinzi yenye cheti cha ubora cha ISO18788. Pia ina vyeti vitatu ambavyo ni pamoja na – ISO 9001 (Ubora), ISO 14000 (Mazingira) na ISO 45000:2018 (Afya na Usalama).

Bw. Sambu alisema wanafurahia ushirikiano kati ya mapuni yake na mashirika ya serikali hasa Jeshi ambalo wanashirikiana nalo katika mafunzo, kuchuja maaskari wakati wa kuajiri, uchunguzi na katika kukabiliana na matukio mbalimbali ya uhalifu.

Alitoa wito kwa makampuni mengine yaige mfano huu kwa kuwajali wafanyakazi wao ikiwemo kuwalipa vizuri kama njia ya kuwapa motisha ya kufanya kazi kwa bidii. “Jambo muhimu ni kuwekeza katika watu na pia kuwapa mafunzo ya mara kwa mara kama linavyoelekeza Jeshi la Polisi,” alisema.

Alisema kampuni hiyo itaendelea kuwekeza katika watu, teknolojia na ubunifu ili kuwapa wateja huduma bora zaidi.

Alisema wamejipanga vizuri kutetea tuzo hiyo mwakani na kuwapongeza waandaaji kwa weledi na kutumia kampuni huru kuendesha tuzo hizo jambo ambalo linafanya wadau waendelee kuwaamini na hata kwa ambao hawakufanikiwa kushinda, walipewa maelezo ya kuridhisha baada ya tathmini kukamilika, jambo ambalo litachochea mabadiliko katika sekta ya ulinzi.

Post a Comment

0 Comments