Header Ads Widget

Mo Aingilia Usajili Wa Rasta Mkameroon Simba

Mo Aingilia Usajili Wa Rasta Mkameroon Simba
Che Fondoh Malone

UONGOZI wa Simba umeweka wazi kuwa hawatoshindwa kumsajili mchezaji yeyote watakayemtaka kulingana na thamani yake kutokana uwepo wa mwekezaji na Rais wa Heshima wa klabu hiyo, Mohammed Dewji.

Simba imetoa kauli hiyo baada ya taarifa kuwa wameshindwa kupata saini ya beki wa Cameroon, Che Fondoh Malone ikidaiwa kuwa anatakiwa na klabu mmoja nchini Zurich.

Hivi karibuni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi wa Simba, Salim Abdallah ‘Try Again’, alikutana na uongozi wa Coton Sport ya Cameroon wiki iliyopita kwa ajili ya majadiliano ya kupata saini ya nyota huyo ambaye muda wowote atasaini mkataba wa miaka miwili kutumikia klabu hiyo ya Simba.

Akizungumza na Championi Ijumaa, Meneja wa Habari na Mawasiliano ya timu hiyo, Ahmed Ally, alisema kuwa kama kuna taarifa ya mchezaji yeyote ambaye anatakiwa na Simba basi wanauwezo wa kumnunua kutokana na bajeti yao kubwa waliyoiweka kwa ajili ya msimu ujao.

“Kama kweli huyo beki anatakiwa au mchezaji yeyote basi Simba haishindwi kumnunua, timu inayomilikiwa na Mo Dewji hatushindwi kumpata, hatusajili wachezaji waliokuwa huru bali tunaenda kuwanunua kutoka ndani ya klabu husika.

“Mapendekezo ya usajili ni kupata beki kuja kusaidiana na Joash Onyango na Henock Inonga kwa msimu ujao wa mashindano, lazima tufanye usajili bora kulingana na mahitaji yetu na mashindano tunayoenda kushiriki,” alisema Ally.

Post a Comment

0 Comments