Nyota wa tenisi wa Marekani Venus Williams anasema atukio la kuanguka kwake lilizima matumaini yake ya kushinda Wimbledon na kumpa "uchungu" na umemuacha "katika mshtuko".
Williams, mwenye umri wa miaka 43, aliteleza mapema katika mechi ya raundi ya kwanza dhidi ya Elina Svitolina wa Ukraine, na kusababisha hofu kwamba huenda akalazimika kuondoka uwanjani akiwa na majeraha.
Bingwa huyo mara tano aliendelea na kumsukuma Svitolina kabla ya kupoteza kwa 6-4 6-3.
"Ilikuwa bahati mbaya kwangu," Williams alisema."Siamini ilitokea. Bado najaribu kuitafakari."Williams, ambaye alianza mechi kwa kufungwa kamba nzito kwenye goti lake la kulia, alionyesha dhamira isiyopungua na ujasiri wa kupambana na matatizo yake kabla ya kushindwa na Svitolina ambaye ni mshindi wa nusu fainali ya 2019.
0 Comments