Yanga: Hatumuogopi Mwarabu Tunalitaka Kombe la Shirikisho
MARA baada ya kutinga fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika na kufahamu kuwa watavaana na timu ya USM Alger ya Algeria, uongozi wa mabingwa wa Ligi Kuu Bara, Yanga umechimba mkwara mzito kuwa haijalishi ni mpinzani gani wanakutana naye kwenye fainali, bali wamejipanga kushinda ubingwa wa mashindano hayo.
Yanga juzi Jumatano walifanikiwa kuibuka na ushindi wa mabao 2-1 mbele ya Marumo Gallants kwenye mchezo wa nusu fainali ya pili ya Kombe la Shirikisho Afrika na kukata tiketi ya kutinga fainali ya mashindano hayo kwa matokeo ya jumla ya ushindi wa mabao 4-1 kufuatia ushindi wa mabao 2-0 kwenye mchezo wa kwanza kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa.
Kwenye nusu fainali ya pili Kombe la Shirikisho Afrika ambayo pia ilipigwa juzi Jumatano USM Alger kutokea Algeria waliwaondosha ASEC Mimosas ya Ivory Coast kwa ushindi wa jumla wa mabao 2-0, baada ya suluhu kwenye mchezo wa mkondo wa kwanza na ushindi wa mabao 2-0 nchini Algeria.
Yanga watavaana na USM Alger kwenye fainali ya kwanza itakayopigwa Mei 28, mwaka huu kwenye Uwanja wa Benjamin Mkapa, Dar es Salaam kabla ya kurudiana Juni 3, mwaka huu nchini Algeria.
Akizungumza na Championi Ijumaa, Rais wa Yanga, Injini Hersi Said alisema: “Haikuwa kazi rahisi kwetu kuweza kufika hapa kutokana na ushindani mkubwa tuliokutana nao hasa kwa kuwa timu yetu haikuwahi kufika hatua kubwa za mashindano haya, nawapongeza wachezaji, benchi la ufundi, viongozi na mashabiki wetu kwa kuwa kwa umoja wetu tumefanikisha lengo hilo.
MASTAA NAO WAAPA
Akizunggumza na Championi Ijumaa, mshamuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa: “Lazima tuhakikishe kuwa tunashinda ubingwa, tayari tumefanikiwa kwenda katika hatua ya fainali sehemu ambayo ni historia kuwa kwa timu hii ya Yanga.
Naye, beki Dickson Job alisema: “Yanga tayari tumefanikisha jambo moja kubwa ambalo ni kuubeba ubingwa wa ligi kuu hili la kombe la shirikisho ni kama tunaona kuwa tumeanza upya, mchezo wetu wa fainali utakuwa ni wa kitofauti sana.
“Hivyo lazima tuhakikishe kuwa tunaucheza mchezo huu kwa kutumia kila mbinu ili tuweze kutwaa ubingwa wetu wa kwanza wa kimataifa na tuandike historia mpya,tunaamini katika uwezo wetu huu na tunaomba mashabiki wazidi kutuombea.”

“Tunafahamu wapinzani wetu ni timu bora, lakini tumejiandaa na kazi kubwa iliyo mbele yetu kuhakikisha tunashinda ubingwa wa mashindano hayo tumekuwa tukisema kila wakati tunaamini inawezekana.”
MASTAA NAO WAAPA
Akizunggumza na Championi Ijumaa, mshamuliaji wa Yanga, Fiston Mayele amesema kuwa: “Lazima tuhakikishe kuwa tunashinda ubingwa, tayari tumefanikiwa kwenda katika hatua ya fainali sehemu ambayo ni historia kuwa kwa timu hii ya Yanga.
“Kwetu tunajisikia fahari kufanikisha hili kwa kuwa tutakuwa sehemu ya historia, hatujaridhidika kufika fainali, sasa tunatamani kushinda kombe kabisa na kulirudisha nyumbani.”
Naye, beki Dickson Job alisema: “Yanga tayari tumefanikisha jambo moja kubwa ambalo ni kuubeba ubingwa wa ligi kuu hili la kombe la shirikisho ni kama tunaona kuwa tumeanza upya, mchezo wetu wa fainali utakuwa ni wa kitofauti sana.
“Hivyo lazima tuhakikishe kuwa tunaucheza mchezo huu kwa kutumia kila mbinu ili tuweze kutwaa ubingwa wetu wa kwanza wa kimataifa na tuandike historia mpya,tunaamini katika uwezo wetu huu na tunaomba mashabiki wazidi kutuombea.”
MATOKEO YA YANGA SHIRIKISHO
Palyoff
Yanga 0-0 Club Africain
Club Africain 0-1 Yanga
MAKUNDI
US Monastir 2-0 Yanga
Yanga 3-1 TP Mazembe
Real Bamako 1-1 Yanga
Yanga 2-0 Real Bamako
Yanga 2-0 US Monastir
TP MAzembe 0-1 Yanga
ROBO FAINALI
Rivers United 0-2 Yanga
Yanga 0-0 Rivers
NUSU FAINALI
Yanga 2-0 Marumo
Marumo 1-2 Yanga
WAFUNGAJI
1.Fiston Mayele Yanga 6
2.Ranga Chivaviro Marumo 6
0 Comments