Header Ads Widget

Hersi Said afunguka kuhusu Yanga SC Leo [May 24, 2023]

Engenia Hersi afunguka kuhusu Yanga SC Leo [May 24, 2023]

Hizi ni Sentensi za Rais wa Yanga Engenia Hersi Saidi akifunguka kwenye Power Breakfast ya Clouds FM kuhusu Yanga SC.

Ni Eng.Hersi Said ambae muda huu anasikika live kupitia 88.5 katika kipindi cha Power Breafast kinachorushwa Clouds akifunguka yale tusiyoyajua kuhusu Yanga SC mpaka kuwa Rais wa Club.

‘Hapo ndio nikaanzisha mpango wa mbadiliko bahati nzuri Dkt Msindo Msola (Mwenyekiti aliyepita ) alikuwa tayari na mawazo ya kuanza kufanya mabadiliko kwahiyo tukasema tunahitaji kuongeza knowledge ndipo tukaileta kampuni ya Laliga’

“La Liga walitupa klabu ya Sevilla ambayo ni klabu ya 3 kwa ukubwa nchini Spain, hawa walikuwa wanatusaidia kutufundisha namna ya uendeshaji wa klabu katika sekta mbalimbali! Tulianza kufanya kazi na Laliga mwaka 2021 na kwa hakika tunaiona faida na matunda ya Yanga kufanya kazi na hawa Sevilla kupitia La Liga!” – Eng .Hersi Said

Mimi Yanga SC niko nayo muda mrefu sana. Nakumbuka 1992 mzee wangu alikuwa anasikiliza mpira kwenye radio kati ya Simba na Yanga ndipo nikagundua mzee wangu ni mpenzi wa Yanga.” – Mhandisi wa Furaha za Wananchi Eng. Hersi Said

“Sikuwahi hata kuwaza kama kuna siku nitakuwa kiongozi wa klabu kubwa ni kitu ambacho kimetokea kutokana na mfululizo wa matukio ambayo yamefanya leo nimekuwa kiongozi wa Yanga. Nilikuwa mwanachama, baada ya hapo GSM ilipoingia katika uwekezaji na Yanga ndipo nikapendekezwa kuwa Rais wa Yanga” –Eng. Hersi Said

“Yanga tupo kwenye mixed mode , 51% Wanachama 49% Mwekezaji , maana yake bado Klabu itakuwa ni ya Wanachama lakini utakuwa umeendelea kufungua boksi la uwekezaji “- Eng.Hersi Said

Aidha Rais wa Klabu ya Yanga SC Hersi Said ameelezea mabadiliko aliyoyafanya baada ya GSM kuingia Yanga SC na yeye kupewa nafasi ya Uongozi.

“Morrison mnayemuona ni zao la usajili wangu straight from Ghana to Tanzania, kabla yakutokea hadi akaenda Simba lakini mimi ndiye niliyemleta Tanzania kwa mara ya kwanza” -Eng. Hersi Said •

“Kuna kauli zipo mitaani kuna watu wanajiita watu wa mpira, hawako kama sisi ma-Engineer ambao tumeenda shule lakini wao sijui wanarasimishwa na nani! Nataka niwaambie hili, Football Club haiendeshwi na Watu wa Mpira, inaendeshwa na Taaluma na nadhani hilo ndio limefanya kwa kiasi kikubwa tuchelewe kufanikiwa katika vilabu vyetu. Unahitaji mtu sahihi kwenye kila idara ili kuiendesha idara husika kiusahihi lakini kwa sisi Yanga nje ya taaluma moja kati ya vigezo vyetu ili tukuajiri ni lazima uwe mwanachama wa Yanga” -Eng. Hersi Said kwenye


Source: Clouds FM 88.5/PowerBreakfast

Post a Comment

0 Comments