Yanga SC inazidi kung’aa katika Soka hususani fainali za Kombe la Shirikisho Afrika.
Sasa Naibu waziri na Mbunge wa jimbo la Muheza mkoani Tanga, Hamis Mwinjuma AKA Mwana FA alizungumza na millardayo.com ameweza kumpongeza Mkurugenzi wa GSM Ghalib kwa uwekezaji aliyoufanya katika timu ya Young Africans kwani ameleta mabadiliko na mapinduzi hususani katika masuala ya soka nchini.‘Ukiizungumzia Yanga bila kumtaja GSM utakuwa umekosea hivyo ningependa kumpongeza Ghalib kwa hapa alipoifikisha Yanga kwani Uongozi wa sasa ni tofauti wa miaka kadhaa iliyopita tumeona mabadiliko hivyo hongera kwake na hii ni chachu kwenye upande wa soka’- Naibu Waziri Hamis Mwinjuma
“Na Jukumu lililobaki kwasasa tuisupport Yanga kwani ndio timu inayowakilisha nchi na ndio timu iliyobeba bendera ya Tanzania katika fainali ya Kombe la Shirikisho Afrika’- Naibu Waziri Hamis Mwinjuma
“Kingine ningetumia fursa hii kumshukuru Rais Samia Suluhu Hassan kwa kuongezea hamasa kwa Klabu ya Yanga ya kiwango cha Fhedha Kutoka Shilingi Milioni 10 hadi 20 kwa kila goili la ushindi litakalofungwa wakati wa mchezo wa fainali pamoja na kutoka ndege itakayowasafirisha wachezaji na Mashabiki kwenda nchini Algeria katika mchezo wa pili wa Fainali ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika utakaochezwa June 3, 2023”– Naibu Waziri Hamis Mwinjuma
Pichani: Kushoto Naibu Waziri wa Utamaduni, Sanaa na Michezo, Hamis Mwinjuma ‘Mwana FA,(wa pili), Mdau wa soka, (tatu), Ghalib Said Mohamed, (Nne), Mbunge wa Morogoro Kusini Mashariki Hamis Taletale maarufu babu Tale .
0 Comments