Waziri wa Habari, Teknolojia ya Habari na Mawasiliano, Nape Nnauye amesema katika mwaka wa fedha 2023/24 Tanzania itarusha satelaiti yake ya kwanza ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za mawasiliano nchini.
Waziri Nape amesema hayo wakati akihitimisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2023/24
“Rais ametangaza hadharani sasa mwaka huu wa fedha Tanzania tutakuwa na satelaiti yetu mwenyezi Mungu atusaidie”
0 Comments