Donald Trump aliyewahi kuwa Rais wa Marekani kuanzia mwaka 2017 mpaka 2021, leo atapandishwa kizimbani katika Mahakama ya Manhattan, New York nchini Marekani, kujibu mashtaka yanayomkabili.
Trump anakabiliwa na mashtaka ya kumnyamazisha kwa kumhonga kiasi kikubwa cha fedha, mwanamama Strormy Daniels anayecheza filamu za ‘kikubwa’, ili asifichue uhusiano wao wa kimapenzi, wkaati wa kampeni za urais mwaka 2016.
Mbali na mashtaka hayo yanayoanza kusomwa rasmi leo, Trump pia anakabiliwa na zaidi ya mashtaka 30 ambayo bado yapo kwenye hatua za uchunguzi.
Wafuasi wa Trump, wamekasirishwa na hatua ya kupandishwa kizimbani, wakidai ni hujuma za kumdhoofisha kisiasa baada ya kutangaza kwamba anataka kugombea tena urais wa nchi hiyo ifikapo 2024.
Ulinzi umeimarishwa katika maeneo mbalimbali jijini New York, ikiwemo mahakama ambayo itatumika kusoma mashtaka yanayomkabili.
Hapo jana Trump alisafiri kwa ndege yake binafsi kutoka Florida mpaka jijini New York kwa ajili ya kuhudhuria mahakamani kusikiliza mashtaka yanayomkabili.
0 Comments