Zaidi ya wakazi 8,500 wa vijiji vya Kichiwa, Maduma na Tagamenda wataondokana na kero ya kukosa maji safi na salama ambayo wanayo tangu Nchi ipate uhuru, hii ni baada ya Wakala wa Maji na Usafi wa Mazingira (Ruwasa) kusaini mkataba wa Sh1.1 bilioni kukamilisha mradi wa maji.
Mbunge wa Lupembe, Edwin Swalle amesema mradi huo umesuasua kwa muda mrefu na amekuwa akipata changamoto za maswali kutoka kwa madiwani na wananchi kuhusu lini utaanza mradi huo.
“Nilipokuwa ziara Kichiwa, Tagamenda na Maduma wananchi ukanda ule wana kero kubwa ya maji ya muda mrefu, wamekuwa wakiulizia sana mradi huu wa maji hata mwaka jana niliulizia kuhusu mradi huu ndani ya Bunge kuhusu mradi huu wa Kitiwa na umuhimu wake kwa wananchi,”
Swalle ameishukuru Ruwasa kwa kuupa kipaumbele mradi huo ambao ni miongoni mwa miradi sita ya maji katika jimbo hilo.
.
.
.
.
.
.
.
0 Comments