MSHAMBULIAJI namba moja kwenye ligi akiwa na mabao 15 huku kwenye Kombe la Shirikisho Afrika hatua ya makundi akiwa na mabao matatu, Fiston Mayele amesema wanahitaji pointi kimataifa ugenini na nyumbani.
Mayele raia wa DR Congo ameweka wazi kuwa kila mechi ambayo wanacheza ni muhimu kushinda ili kupata pointi tatu ambazo wanazihitaji.
Ikumbukwe kwamba bao lake alilofunga dhidi ya US Monastir Uwanja wa Mkapa akitumia pasi ya mshikaji wake Kennedy Musonda limechaguliwa kuwa bao bora mchezo wa tano kwenye Kombe la Shirikisho Afrika.
Akizungumza na Championi Jumamosi, Mayele alisema wana mechi ngumu za kucheza lakini wanachohitaji ni kupata pointi tatu kila wanaposhuka uwanjani.
“Kikubwa ni kupata pointi tatu iwe nyumbani ama ugenini, tunajua siyo kazi nyepesi ambacho tunakifanya ni kushirikiana na kupambana kupata matokeo mazuri kwenye mechi zetu ambazo tunacheza.”
Aprili 2, 2023 Yanga inatarajiwa kucheza mchezo wa kukamilisha mzunguko wa sita kwenye kundi D dhidi ya TP Mazembe.
0 Comments