Header Ads Widget

DNA: Diamond amesaidia kuukuza muziki wa Afrika Mashariki (Video)



Msanii mkongwe wa muziki kutoka nchini Kenya DNA amefunguka namna msanii wa muziki wa Bongo Fleva @diamondplatnumz alivyopenya katika soko la muziki ukanda wa Afrika Mashariki hasa nchini Kenya.

DNA kupitia Podcast yake ya DNA Mister Dreams ameeleza kwa urefu tangu mwanzo @diamondplatnumz anaanza muziki na nyimbo ya KAMWAMBIE, MBAGALA na zingine.

Kipindi @diamondplatnumz anaanza muziki tayari DNA alikuwepo kwenye industry hivyo aliuona ukuaji wa @diamondplatnumz tangu mwanzo.

Kipindi @diamondplatnumz anaanza muziki kwa ukanda wa Afrika Mashariki muziki ulishikiliwa na Kenya ikiongozwa na wasanii kama Juakali, Nonini, Wyre, Amani, DNA, Longomba na wengine.

DNA anasimulia namna @diamondplatnumz alivyokua Kibiashara na kuwazidi wasanii wengine.

Anasimulia kuanzia menejiment, lebo, Matamasha, alivyo-set level na mengine.

“Kuna kipindi Kenya walikuwa wanazuia nyimbo za nje lakini mwa @diamondplatnumz walishindwa, unakuta dada anaenda club analipia anamwambia DJ niwekee ngoma ya @diamondplatnumz wasanii wa Kenya walikuwa wamenunua kama wamekula ndimu.” DNA.


DNA pia amezungumzia suala la lugha kwa @diamondplatnumz kwenda kujifunza Kiingereza ili kuboresha biashara yake ya muziki lakini kutafuta meneja mwenye Connection ambaye ni @sallam_sk

NB: Hii ilikuwa ni Episode ya mwezi wa 12 kwenye DNA Mister Dreams.

Post a Comment

0 Comments