Baada ya kuwepo taarifa za kwamba huenda ushindi wa Rais mteule wa Marekani Donald Trump ungetenguliwa, hatimaye wajumbe wa Baraza la Uchaguzi la Marekani, (Electoral College) limepiga kura na kutoa tamko rasmi kuwa ushindi wa mwanachama huyo wa Republican ni halali.
Donald Trump na atakayekuwa makamu wake Mike Pence wameidhinishwa na baraza hilo kwa ushindi wa kura zaidi ya 270 ikiwa ni wiki sita baada ya kupita uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo November 8, 2016 japokuwa kwenye upande wa kura za wananchi wa kawaida bado Hillary Clinton ameendelea kuongoza baada ya kuongeza kura zaidi ya milioni 3 baada ya matokeo kutangazwa.
Kupitia kurasa zao za Twitter, Donald Trump na makamu wake Mike Pence wameonesha furaha yao baada ya kuthibitishwa kwa ushindi wao.
0 Comments