Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda akizungumza na wamiliki wa kumbi za starehe, bendi na wadau wa burudani leo.
Mdau wa burudani, Juma Mbizo akizungumza jambo wakati wa mkutano wa leo.
Msanii Hemed Maliyaga ‘Mkwere’ naye alikuwepo.
Wadau mbalimbali wa burudani wakifuatilia mkutano huo.
Wanahabari wakichukua matukio wakati wa mkutano huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar, Paul Makonda akiwasili eneo la mkutano mbali na mvua kubwa iliyokuwa inanyesha leo.
Mwanamuziki Khadija Kopa wakati akielekea kwenye ukumbi wa mkutano na Mkuu wa Mkoa wa Dar.
MKUU wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda, leo alizungumza na wamiliki wa kumbi za starehe, bendi na wadau wa burudani ambapo mada kubwa iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu ni utekelezaji wa amri ya kufunga kumbi za starehe saa sita usiku.
Akiichambua hoja hiyo kwenye mkutano uliofanyika Ukumbi wa Vijana Kinondoni, Makonda alisema hawezi kubadilisha agizo hilo kwa kuwa yeye anatimiza wajibu wake kwa kusimamia sheria na atakayekiuka atakiona.
“Siwezi kutengua sheria hiyo mpaka itakapofanyiwa marekebisho bungeni, kwani kufanya hivyo naweza kuonekana natumia vibaya madaraka yangu au pengine nimepewa kitu fulani ili kunishawishi kuwaruhusu kuvunja sheria.
Kumbi zinazotakiwa kutumika muda wowote ni zile zenye vibali maalum vya Night Club” alisema Makonda.
Makonda alisema hayo na hakutaka kupokea swali lolote katika kikao hicho lakini aliwasisitiza wajumbe wa kikao hicho kujadiliana mapendekezo yao na kumpelekea ili nae ayapeleke kwa wahusika ili yakionekana kufaa yakajadiliwe bungeni na kubadili sheria hiyo.
0 Comments