Header Ads Widget

Sentensi 6 za Naibu Waziri Hamisi Kigwangalla baada ya kufungia wafanyakazi nje ya geti Dec 18.. (+Picha)




Ijumaa ya December 18 2015 inakuwa siku ya sita tangu Mawaziri na Manaibu wao walioteuliwa na Rais Magufuli waapishwe Ikulu Dar es Salaam… kwenye list ya Baraza hilo, yuko pia Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Dk. Hamisi Andrea Kigwangalla, ambaye pia ni Mbunge wa Jimbo la Nzega Tabora.

Nimepita kwenye ukurasa wake Instagram @hamisi_kigwangalla, ambapo amepost picha na ujumbe unaosomeka hivi >>> ‘Tumefunga geti la ofisi za Wizara ilipofika saa 1:30 asubuhi. Tunataka watumishi wa Wizara wawahudumie wateja wetu Kwa tija na ufanisi‘



Sentensi nyingine za Naibu Waziri zinasomeka hivi >>> ‘Mimi nitawajibika kazini. Kila mtu atapaswa kuwajibika. Haya ndiyo mahitaji ya wakati huu. Leo nimefungia wachelewaji kazini nje ya geti. Nitaendelea kushughulika na watoro na watorokaji. Nasubiri ripoti ya watendaji kuhusu trend ya watumishi wote watoro, wachelewaji kisha nichukue hatua stahiki! Ili kazi ziende ni lazima tuweke nidhamu ya kazi Na uwajibikaji maofisini.’ >- @hamisi_kigwangalla





Picha zote >>> Issa Michuzi Blog

Post a Comment

0 Comments