Header Ads Widget

HAWA NI WENGINE WALIOANDAMANA NA NGURUWE HUKO KAMPALA NCHINI UGANDA


Ile ishu ya raia mbalimbali wa Uganda kutumia Nguruwe wadogo kwenye maandamano kuwasilisha ujumbe wao au kuwekea msisitizo kwenye matatizo yanayowasumbua imerudi tena kutumika.

Vijana wawili ambao ni Mwanamke mmoja na Mwanaume mmoja walikamatwa na Polisi pamoja na gari walilokua wakitumia baada ya kuonekana wakitupa Nguruwe wanne waliopakwa rangi ya njano karibu na kanisa la Wakole kwenye jiji la Kampala.

Japo haijajulikana sababu yao ya kuwatupa hao Nguruwe ilikua nini, mmoja kati ya Nguruwe hao alikua kavishwa kofia na mwingine kabandikiwa maandishi ambapo wengi wanaamini Nguruwe hizo zilikua kwenye mpango wa kusanifu tamasha la Kampala City Festival.


Hii sio mara ya kwanza kuona watu wakiandamana na Nguruwe kwenye jiji la Kampala ambapo siku kadhaa zilizopita kuna watu waliingia matatizoni na kukamatwa na Polisi kutokana na kuandamana na Nguruwe mpaka kwenye bunge la nchi hiyo kusisitizia matatizo yao kusikilizwa.

Post a Comment

0 Comments