Video vixen maarufu wa Bongo Agnes Gerald maarufu zaidi kwa jina la Agnes Masogange ambaye kwa miezi kadhaa sasa amehamishia makazi yake Afrika Kusini, amebadili jina na huenda akawa raia wa huko!
Kupita Instagram mrembo huyo mwenye umbo ‘matata’ alianza kwa kupost picha ya pasi ya kusafiria ya Afrika Kusini kama ishara kwamba amepata uraia mpya wa nchi hiyo.
Kuthibitisha kile ambacho kila mmoja alifikiria (kuwa amebadili uraia) Masogange baada ya muda mfupi aliandika kuhusu kubadili na jina pia. “My new name is thando not Agnes any more”
Hivi karibuni Mwandishi alikutana uso kwa uso na Agness Thando jijini Durban, Afrika Kusini kwenye tuzo za MTV MAMA 2014, na katika mahojiano alisema kuwa kwa sasa amehamia kabisa Afrika Kusini na makazi yake yako jijini Johannesburg.
Kutokana na sheria za Tanzania ambazo haziruhusu uraia wa nchi mbili, hii inamaanisha Thando si mbongo tena....
0 Comments