Tukio hilo la kusikitisha limetokea jana saa saba mchana katika kitongoji cha Kashampa kijiji cha Nhelegani kata ya Kizumbi ambapo mwili wa marehemu ulikutwa kichakani.
Kaimu mganga mfawidhi wa hospitali ya Mkoa wa Shinyanga Dkt Daniel Maguja amesema vipimo vinaonesha kuwa mtoto huyo alibakwa na kutobolewa macho.
Kamanda wa polisi mkoani hapa Justus Kamugisha amethibitisha kutokea kwa tukio hilo na kuongeza kuwa chanzo cha tukio hilo kinachunguzwa huku akitoa wito kwa wananchi kutoa taarifa zitakazosaidia kuwabaini na kuwakamata wauaji ili hatua za kisheria zichukuliwe.
Na Kadama Malunde-Shinyanga
0 Comments