Halida Ng’anguli akiwa ameanguka nje ya choo katika uwanja wa Samora kabla ya kufariki dunia (picha na habari na Francis Godwin Blog)
kaimu sheikh wa mkoa wa Iringa Abubakar Chalamila
WAKATI waislamu nchini jana wameungana na waislamu wenzao duniani kuswali sala ya Iddi mkoani Iringa swali hiyo imemalizika vibaya kufuatia kifo cha muumini mwenzao Halida Ng’anguli mkai wa Mwangata C ambae ni shangazi wa manahabari wa gazeti la majira Iringa Zuhura zuhkeri kufariki dunia baada ya masaa machache toka aanguke chooni uwanja wa Samora.
Tukio la kuanguka kwa mwanamke huyo lilitokea majira ya saa tatu asubuhi wakati waumini wa dini ya Kiislamu ambao walikuwa wakiswali pamoja katika uwanja wa samora mjini Iringa kumaliza swala na kuanza maandalizi ya kuondoka uwanjani hapo kabla ya mmoja kati ya viongozi kwa kutumia kipasa sauti kutangaza tukio la kuanguka kwa mwanamke huyo huku akiwataka wanawake kwenda eneo la tukio katika vyoo vya wanawake ili kutoa msaada zaidi.
Hata hivyo jitihada za waumini hao wanawake pamoja na askari waliokuwepo uwanjani hapo zilifanikisha kumkimbiza mweanamke huyo hospitali ya Rufaa ya mkoa wa Iringa kwa matibabu zaidi.
Ibada ya idd ikiendelea katika uwanja wa Samora mjini Iringa
Mbali ya jitihada kubwa za madaktari wa Hospitali hiyo kutaka kunusuru maisha yake bado hali ilionekana kuwa mbaya zaidi kutoka na tatizo ya ugonjwa wa kisukari lililokuwa likimsumbua .
Yapata majira ya saa 4 usiku mwanamke huyo alifariki dunia wakati akiendelea kupatiwa matibabu Hospitalini hapo.
Mwenyekiti wa CCM Iringa mjini Abed Kiponza wa tatu kushoto akishiriki ibada ya Iddi
Mwanahabari Zuhura Zukheri wa tatu kushoto akiwa na mwanahabari Clement Sanga kulia na mmiliki wa mtandao huu mzee wa matukiodaima wakipata nyama wakati wa ziara ya kuelekea mikoa ya kaskazini kutangaza utalii wa ndani .
Akithibitisha kutokea kwa kifo hicho Shangazi wa marehemu mwanahabari Zuhura Zukheri alisema kuwa shangazi yake alifariki majira ya saa 4 akiwa katika matibabu na kuwa toka alipofikishwa Hospitali hapo hari yake ilikuwa mbaya na hakuweza kupata nafuu.
Zuhura alisema kuwa tatizo kubwa lililokuwa likimsumbua ni ugonjwa wa Kisukari na kuwa shughuli za mazishi zimepangwa kufanyika leo ambayo ni siku ya Iddi pili majira ya saa 10 jionini .
Uongozi wa chama cha waandishi wa habari mkoa wa Iringa (IPC) unaungana na familia ya mwanahabari huyo Zuhura Zukheri katika wakati huu mgumu wa maombolezo ya kifo cha mpendwa wetu huyo
0 Comments