Mkuu wa wilaya ya kahama mh Benso Mpesya akifungua mafunzo hayo.
Mkuu wa wilaya ya kahama mkoani shinyanga Mh Benson Mpesya leo amefungua rasmi mafunzo ya nishati itokanayo na mionzi ya jua ,yaliyoandaliwa na wakala wa nishati vijijini (REA).
Ufunguzi wa mafunzo hayo ya siku saba umefanyika katika ukumbu wa kartas wilayani Kahama mkoani shinyanga ,lengo ikiwa ni kuwapatia vijana 20 kutoka halmashauri ya Msalala ujuzi wa kufunga nishati jadilifu(solar power).
kaimu afsa elimu wilaya ya msalala SELEKA NTOBI
Aidha mpesya amewataka vijana kuzingatia wanayofundisha na wakufunzi pamoja na kuyaheshimu mafunzo hayo ,kwani wakiyazingatia na kuyaelewa watakuwa wamejipatia ajira.
Kwa upande wake kaimu afisa elimu halmashauri ya msalala Seleka Ntobi ,amesema hiyo ni fursa kwa vijana 20 wa halmashauri hiyo kupata ujuzi ,kwani wataalamu wa ufungaji wa nishati jadilifu ni wachache katika halmashauri hiyo.
Kupitia mafunzo hayo Seleka ameongeza kuwa shule kumi na sita za halmashaur ya msalala zitafungwa nishati hiyo.
Naye mkurugenzi wa ufundi kutoka kampuni ya REX ENERGY ambao ndio waendeshaji wa mafunzo hayo Eng John Maijo ,amesema endapo vijana hao watayazingatia mafunzo wanayopatiwa na wakufunzi ,yatawanufaisha kwani pia wanaweza kujiajiri wenyewe kupitia mafunzo hayo.
Mafunzo hayo ya siku saba yaliyoandaliwa na wakala wa nishati vijijini (REA) na kuendeshwa na wakufunzi kutoka kampuni ya REX ENERGY kutoka Dare s salaam yameanza leo na yatamalizika tarehe 21 mwezi huu.
mwanasemina akitoa jambo
0 Comments