Kocha mkuu wa zamani wa timu ya Taifa, taifa Stars Marcio Maximo amesaini mkataba wa kuwa kocha mkuu na timu ya Yanga kwa muda wa miaka miwili. makubaliano hayo yamefikiwa jana, wakala anaye mwakilisha Ally Mleh wa kampuni ya Manyara Sports Management amethibitisha hilo.
"Ni kweli kocha Marcio Maximo amekubali kuingia mkataba na timu ya Yanga ambapo anatarajiwa kuanza kazi rasmi tarehe 27/06/2014 ambapo atafuatana na msaidizi wake Leonardo Neiva. Mazungumzo ya makubaliano hayo yalichukua muda mrefu kidogo hatimaye tumefikia makubaliano.Tunashukuru mungu kila kitu kimekamilika.
Kwa niaba ya Marcio Maximo napenda kuushukuru uongozi wa klabu ya Yanga, shukrani za pekee kwa mwenyekiti wa Yanga ndg Yusuf Manji na makamu wake Clement Sanga, kwa kweli wameonyesha umakini na professional kwa muda wote wa majadiliano. Nawaomba wachezaji,wanachama na wapenzi wote wa yanga tumpe ushirikiano.
Baada ya kumaliza mkataba wake wa kuifundisha Taifa Stars nchini aliingia mkataba na timu kubwa nchini brazil mpaka mkataba wake ulipoisha.Kwa wakati huu kulikuwa na mazungumzo na timu mbalimbali Zilizotoa ofa nchini China, Ethiopia na Afrika kusini lakini Yanga wamefanikiwa kumnasa kocha huyo.
Maximo anatarajia kuwasili LEO siku ya Alhamis saa saba mchana
Maximo ilikuwa awasili nchini baada ya fainali za kombe la dunia lakini kutokana na mkataba alioingia na Yanga imebidi afupishe mkataba wa kazi ya 'commentator' aliyokuwa akiifanya nchini Brazil ili awahi kuandaa program zake Yanga.
0 Comments