Mchekeshaji wa muda mrefu Amri Athuman 'Mzee Majuto' ametoa kali ya mwaka baada ya kusema kuwa maisha yake ni komedi tosha kutokana na kumvunja mtu mbavu bila kujali yuko mahala gani....
Akizungumza na mwandishi wetu, Mzee Majuto alisema yeye hutoa shoo muda wowote bure bila kujali yuko katika wakati gani kwani maisha yake ni komedi tupu...
"Maisha yangu ni komedi tosha,siwezi kuacha kuchekesha.Wakati mwingine si kwa kupenda bali huwa najikuta tu nimefanya hivyo , inabidi watu wanizoee tu....
"Huwa sina nia ya moja kwa moja kuchekesha watu, lakini kumbe kauli zangu huwavunja mbavu.Sijisikii vibaya kwa hilo, najivunia kuendelea kuwa msanii ninayekubalika hadi umri huu," alisema mzee Majuto
CREDIT: EDWINMOSHI.COM
0 Comments