Shamrashamra za harusi ya mastaa wakubwa wanaomake headlines kwa sasa nchini Marekani na duniani kwa ujumla Kim Kardashian na Kanye West wanaotarajia kufunga ndoa hii leo zimezidi kushika kasi baada ya jana kufanya pre wedding dinner iliyotikisa mitaa ya jiji la Paris Ufaransa na kuhudhuriwa na ndugu pamoja na marafiki wa couple hiyo matata.
Wapenzi hao wanaojulikana kwa jina moja la Kimye waliburudika kwa pamoja na marafiki zao katika hafla hiyo iliyowapa nafasi ya kujikamilisha zaidi kwa ajili ya harusi.
Ingawa ‘Best man’ wa Kanye West Jay Z pamoja na mkewe Beyonce hawakuwepo katika tukio hilo lakini wanatarajia kuhudhuria harusi.
Millard Ayo.com itakushushia info zote kuhusiana na harusi hiyo ili wewe shabiki wa Kim na Kanye uweze kuona couple yako maarufu ilichofanya.
Hizi hapa baadhi ya picha za Pre wedding ambazo ziko kwa ajili yako.
0 Comments