Header Ads Widget

Kiongozi wa upinzani Uganda kazingua tena, Polisi hawajamvungia aisee..!



Polisi wamemkamata kiongozi wa chama kikuu cha upinzani Kizza Besigye, ambaye ni mgombea wa urais nchini Uganda, siku moja baada ya uchaguzi kufanyika.

Kizza Besigye aliwekwa kizuizini wakati polisi walipovamia Makao Makuu ya chama chake, katika mji mkuu wa Kampala. Besigye alikuwa akitaka kuitisha mkutano na waandishi wa habari. Mabomu ya machozi yamelipuliwa nje ya jengo la makao makuu ya chama hicho.

Matokeo rasmi ya uchaguzi kwa karibu nusu ya vituo vya kupigia kura yametangazwa, Rais Yoweri Museveni anaongoza. Museveni anawania kwa awamu ya tano, baada ya miaka 30 madarakani.



Kwa mujibu wa wa matokeo ya awali yaliyotolewa na tume, Museveni anaongoza kwa 62% ya kura, wakati Besigye ana 33% ya kura.

Polisi bado hawajatoa kauli juu ya sababu ya kukamatwa Besigye. Ikiwa hii ni mara ya tatu katika muda wa wiki moja kwa Kiongozi huyo kuwekwa kizuizini.

Upigaji kura bado unafanyika katika baadhi ya maeneo ambayo vifaa vya kupigia kura vilichelewa kuwasili kwenye vituo, ambapo vituo hivyo havikufunguliwa kabisa siku ya Alhamisi.

SOURCE: BBC

Post a Comment

0 Comments