Vitendo vya ukatili dhidi ya watoto vimeendelea katika jamii ambapo mtoto mmoja anayekadiriwa kuwa na umri wa miaka sita ameokolewa na watoto wenzie waliomkuta amefungwa kamba mikono na miguu katika eneo la Nyasaka B wilayani Ilemela jijini Mwanza
Hali hiyo imezua taharuki miongoni mwa majirani wa eneo hilo wanaomtuhumu mama mkubwa wa mtoto huyo aliyetambulika kwa jina la Nyanzugu Werema kumtendea unyanyasaji wa mara kwa mara mtoto huyo na kuamua kumpeleka kituo cha polisi ili sheria ichukue mkondo wake
Kwa sasa watoto wanaonekana kutambua haki zao hali ambayo imeokoa maisha ya mtoto huyu anayedaiwa kufanyiwa unyanyasaji wa kutopata haki muhimu za watoto ikiwemo chakula,malazi na elimu
Wananchi walikusanyika katika kituo kidogo cha polisi cha Buzuruga eneo la Mtena B wameelezea jinsi walivyopata taarifa za kufungwa kamba kwa mtoto huyu.
Mama mkubwa anayedaiwa kumtendea unyanyasaji mtoto huyu yeye anadai afya ya mtoto huyu si kwa kunyanyaswa bali ni kutokana na ugonjwa jambo ambalo linapingwa vikali na badhi ya majirani
Eneo la Nyasaka B mahali anapoishi Nyazungu sehemu hii inatajwa kuwa sehemu ya mtoto huyu kulala,huku chakula akisubiri mama Nyazungu na familia yake wamalize kula ndipo naye apate chochote
0 Comments