Header Ads Widget

MASIKINI!! HURUMA IKO WAPI??; HUYU NDO MWANAMKE ALIYEPIGA MAGOTI HOSPITALI KUBEMBELEZA APATIWE DAWA ZA MAUMIVU KABLA YA KIFO CHAKE.



Unaweza kudhani matukio haya hutokea katika hospitali za kawaida tu. Hii ni ya kusikitisha zaidi, Picha hii ya mwisho inamuonyesha mwanamke mmoja aliyekuwa amezidiwa hospitali na akashindwa kupatiwa dawa
hadi kuamua kupiga magoti akibembeleza apatiwe dawa ya maumivu tu kutokana na kuzidiwa kwake lakini wauguzi hawakumsaidia chochote hadi umauti ulimkuta

Siku mbili baada ya kutelekezwa na maafisa wa hospitali, mwanamama huyo Margaret Lamberty alipoteza maisha baada ugonjwa wake unaotibika kumzidi kutokana na kushindwa kupatiwa msaada.
Margaret alifikishwa hospitali ya chuo kikuu cha A&E Kaskazini mwa Staffordshire na wanafamilia yake akiwa na maumivu makali ya tumbo, Mtoto wake kike aitwaye Laura amesema kuwa baada ya kufika hospitalini hapo wauguzi walikuwa wakimuangalia tu bila kumpa msaada wowote ndipo mama yake akaamua hadi kupiga magoti akiwaomba wampatie dawa ya maumivu lakini hakusikilizwa na mtu.
Baada ya kifo cha mwanamke huyo, Familia inapanga kuishtaki hospitali hiyo kwa kushindwa kutimiza wajibu wao hadi kusababisha kifo cha ndugu yao.

Post a Comment

0 Comments