Msanii maarufu wa Kenya, Nyota Ndogo amejikuta akimwaga machozi kutokana na aibu aliyoipata baada ya kundi kubwa la watu kumshuhudia akiwa uchi wa mnyama huku akijipaka mafuta pasi yeye kujua.....
Nyota Ndogo alikumbwa na dhahama hiyo alipokuwa aki perform katika show moja nchini Kenya hivi karibuni.
Kwa mujibu wa maelezo ya msanii huyo aliyoyatoa katika ukurasa wake wa facebook ni kuwa, akiwa katika Show hiyo, mwenyeji wake alimpatia chumba kwa ajili ya kubadili nguo, akaingia na kuvua nguo zote na kisha kuanza kujipamba. Amekuja kustuka kuwa anachunguliwa na watu baada ya kusogolea kioo kilichokuwa ndani ya chumba hicho ambapo aliwaona watu hao wakimwangalia....
"Yani nimekwenda show.nikapewa chumba chakubadili nguo.nimevua nguo zote najipaka mafuta pole pole kumbe najiangalia kwa kioo kumbe upande wapili naoneka kila kitu.yani nimekosa amani...aibu nilio iona mungu ndio anajua.sijui wamechukua video..haya ngoja tusubiri," amendika kwa uchungu msanii huyo
Msanii huyo amemtwisha zigo la lawama mwenyeji wake aliyempatia chumba hicho ili hali akijua kinaonekana kwa nje
"Hapana nilibakisha cha ndani na nyonyo ilikua na nguo pia.kitu sielewi ni alienipeleka kubadili nguo ina maana hakujua nje naonekana?maana aliambia kioo hiki jiangalie mpaka miguu."Ameandika Nyota Ndogo na kuongeza
"Kuajulisha tu ili kama walichukua video mukiiona mujue niliwataarifu"
Aidha, Nyota Ndogo aliutumia pia ukurasa huo kuwasihi watu hao wasitoe picha zake za uchi au video kama walirekodi ili kumtunzia heshima mbele ya watoto wake
"Wafikirie wanangu," Ameandika msanii huyo.
0 Comments