Kocha Jose Mourinho Afungiwa Mechi 4 Za UEFA kwa kosa la Kumyanyasa Muamuzi
MENJA wa Roma, Jose Mourinho ambaye ni Meneja wa zamani wa Chelsea, Manchester United na Tottenham amefungiwa kwenye mechi 4 za UEFA baada ya kumyanyasa muamuzi Anthony Taylor katika Fainali za Ligi ya Uropa.
Video kadhaa zilimuonyesha Mourinho akimfuata Taylor na kumuita “fedheha” na kurusha matusi kadhaa kwake. Tukio hili lilifanyika katika eneo la kuegeshea magari baada ya timu yake kushindwa na Sevilla kwenye fainali ya Ligi ya Europa mwezi ulipita.
Baadaye, video nyingine ilimuonyesha Taylor akisumbuliwa na mashabiki wenye hasira katika Uwanja wa Ndege wa Budapest suala ambalo lilikemewa vikali na Ligi ya England.
Jopo la nidhamu la UEFA limemkuta Mourinho na hatia ya kutumia lugha ya kinyanyasaji dhidi ya afisa wa mechi hiyo.
Sambamba na kufungiwa huko, UEFA imewapiga Roma faini ya euro 55,000 na itaipiga marufuku kuuza tiketi kwenye mechi yao ijayo ya ugenini katika ligi ya Uropa.
Aidha, klabu ya Roma imetakiwa kuwasiliana na Shirikisho la soka la Hungary ili kulipa fidia za uharibifu uliosababishwa na mashabiki wao kwenye uwanja wa Puskas.
Wakati huohuo, klabu ya West Ham imepigwa faini ya euro 58,000 huku mashabiki zao wakifungiwa kutokuwemo kwenye mchezo wao wa kwanza ligi ya Uropa (ugenini) katika msimu ujao.
Vifaa mbalimbali vilirushwa wakati waliposhinda kwenye fainali za ligi ya Europé Conference na vilevile uwanja ulivamiwa hali iliyopelekea mlinzi wa Fiorentina , Cristiano Biraghi kuumia kichwani kutokana na kitu kilichorushwa kutoka kwa mashabiki.

0 Comments