Header Ads Widget

Huyu Hapa Kocha Mpya Wa Yanga Miquel Angel Gamondi

Huyu Hapa Kocha Mpya Wa Yanga Miquel Angel Gamondi
KLABU ya Yanga imemtambulisha Muargentina, Miguel Ángel Gamondi (59) kuwa kocha wake mpya akirithi mikoba ya Mtunisia, Nasredeen Mohamed Nabi aliyeondoka.
Kocha huyo ametambulishwa mchana huu katika Mkutano Mkuu wa mwaka wa klabu ukumbi wa Kimataifa wa Mikutano wa Julius Nyerere (JNICC) Jijini Dar es Salaam.

Gamondi, ambaye ni mzaliwa huyo wa mji wa Olavarría, alianza kama mchezaji katika klabu ya nyumbani kwao, Ferrocarril Sud na alipostaafu mwaka 1987 akahamia kwenye ukocha.
Alianza kufundisha klabu za kwao Ferrocarril Sud, Racing, El Fortín, San Martín de Tucumán na Racing Club de Avellaneda kabla ya kuja barani Afrika.

Mwaka 2000 alikuwa Msaidizi wa Muargentina mwenzake, Oscar Fulloné katika klabu ya Al-Ahly ya Libya kabla ya kuhamia naye timu ya taifa ya Burkina Faso Desemba mwaka 2001.
Akawa pia Kocha Msaidizi wa ASEC Mimosas ya Ivory Coast, Wydad Casablanca ya Morocco, Espérance na Étoile du Sahel za Tunisia kabla ya kuwa Msaidizi wa Muargentina mwenzake mwingine, Ángel Cappa katika klabu ya Mamelodi Sundowns ya Afrika Kusini mwaka 2005.

Kwa mara ya kwanza alikuwa Kocha Mkuu wa klabu ya Platinum Stars ya Afrika Kusini Desemba mwaka 2007 na kuiongoza timu hiyo kufika Hatua ya 16 Bora ya Kombe la Shirikisho Afrika mwaka 2008.
Baadaye akazifundisha CR Belouizdad na USM Alger za Algeria, Ittihad Kalba na Al Urooba za Falme za Karabu (UAE), Hassania Agadir, Wydad AC na Ittihad Tanger za Morocco kama Kocha Mkuu na kwa mafanikio.

Mara ya mwisho alifundisha Ittihad Tanger ambako alifukuzwa Aprili mwaka jana kwa pamoja na Msaidizi wake, Tarek Chihab.

Post a Comment

0 Comments