Kiongozi Azimio la Umoja Raila Odinga kuhinikiza kwa Rais Ruto kuachana na muswada wa fedha wa 2023
Kiongozi wa Muungano wa Kenya Raila Odinga amemtaka Rais William Ruto kuachana na msukumo wake wa Mswada wa Fedha wa 2023 huku kiongozi huyo wa upinzani akisema mswada huo umezua wasiwasi usio wa lazima miongoni mwa Wakenya na kwamba ni lazima Rais auache na kuwaomba Wakenya msamaha.Mwanasiasa huyo mkongwe, ametoa wito kwa Rais Ruto kuachana na mpango huo anaosema unalenga kuwaongezea wakenya mzigo haswa wakati huu wanapokabiliwa na hali ngumu ya maisha.
Muungano wa Azimio umetishia kutumia njia zengine ambazo zitawahusisha raia ikiwemo maandamano, iwapo rais Ruto atawashawishi wabunge kuunga mkono muswada huo.
“Tunamtaka Ruto ajishushe, aondoe mswada huu, aombe msamaha na kuomba Wakenya msamaha kwa wasiwasi uliosababisha na kuanza upya,” akasema Bw Odinga.
‘If Ruto insists on this Bill, this country will go into full recession. This Bill requires and must get fierce resistance’.
Kiongozi huyo wa Upinzani pia alisema nchi inapitia nyakati ngumu na kutoza ushuru zaidi kwa Wakenya kutawalemea.
Bw Odinga alisema tangu serikali ya Kenya Kwanza kuchukua mamlaka mwaka jana, deni la nchi limepanda kutoka Sh8.71 trilioni hadi Sh9.3 trilioni.
Aidha katika hatua nyingine Odinga, ameishauri Serikali kupunguza ukubwa wa serikali, kuziba mianya inayochangia kupotea kwa fedha za umma, kupunguza safari za watumishi nje ya nchi, kupunguza marupurupu ya mawaziri na makatibu katika wizara.
Hizi majuzi rais Ruto alisema anasubiri kuona wabunge watakaopinga muswada huo, hatua ambayo wachambuzi wa siasa wanasema inalenga kuwashurutisha.
0 Comments