Header Ads Widget

Inter Milan vs AC Milan: Kwanini Derby hii ya klabu bingwa Ulaya ni kama vita

Inter Milan vs AC Milan: Kwanini Derby hii ya klabu bingwa Ulaya ni kama vita


Kulikuwa na Rui Costa na kulikuwa na Marco Materazzi. Mreno huyo maridadi akibeba uzito wa kiwiko cha mpinzani wake .

Utulivu katikati ya machafuko hayo wakati jozi ya wapinzani wa kandanda walipotulia ili kutafakari juu ya ukuta mweusi wa moshi mwekundu na miali inayowaka.

"Kila mtu alizingatia miale ya moto, kwenye moshi," mpiga picha Stefano Rellandini, ambaye alinasa picha hiyo ya kitambo miaka 18 iliyopita, aliambia BBC Sport. "Lakini karibu na katikati ya uwanja niliona wakati fulani.

"Materazzi alipewa jina la utani kama mchinjaji; yeye si mchezaji mpole. Rui Costa alikuwa kinyume chake - mpole zaidi, kisanii zaidi katika mchezo wake. Kwa sekunde kadhaa Materazzi aliweka kiwiko chake kwenye bega la Rui Costa.

"Kwa hiyo nilipoona hivyo, nilipiga picha. Nina fremu moja tu katika picha hiyo. Huo ulikuwa wakati huo."


Picha hiyo ina urithi wake, lakini pia ilinasa mwisho wa mechi ya hivi majuzi ya AC Milan na Inter Milan ya Ligi ya Mabingwa; robo fainali ya 2005 ambayo ilitibuka baada ya moto na vitu vingine kurushwa kwenye uwanja wa San Siro kutoka kwa sehemu ya mashabiki wa Inter, mmoja akimpiga na kumjeruhi kipa wa Milan Dida.

Dakika 73 za mchezo wa marudiano zilichezwa, mwamuzi aliachana na mchezo huo na mechi hiyo iakazawadiwa Milan ambao walikuwa wanaongoza kwa jumla ya mabao 3-0.

"Hali ya usiku huo ilikuwa kama kila wakati unapocheza na AC Milan na Inter derby huko San Siro," anasema Rellandini, ambaye alikuwa akifanya kazi na Reuters wakati huo.

"Siku zote ni nguvu. Hawapigani sana, lakini upangaji wa mashabiki ni mkubwa na mzuri, kwa hivyo unaweza kuhisi, hata kama wewe si mchezaji.

"Unapoweka miguu yako uwanjani, unaweza kuhisi kuwa sio mechi ya soka tu. Ni kitu kingine zaidi.

"Uko karibu sana na wachezaji. Ilikuwa hali nzuri; kulikuwa na mihemko.

"hali ilitibuka pale walipokataa bao la Esteban Cambiasso. Bao hilo lilibadilisha kabisa hali hiyo.

"Wafuasi wa Inter Milan walikuwa wakichanganyikiwa. Walianza kurusha vitu chini, moto, na waliendelea kufanya hivyo kwa takriban dakika 15 au 20. Ilikuwa kama vita."

Mvutano ulikuwa umeanza. Milan ilikuwa imeiondoa Inter kwenye michuano hiyo miaka miwili iliyopita kwa mabao ya ugenini, licha ya mechi zote mbili za nusu fainali kumalizika kwa sare kwenye Uwanja wa San Siro. Milan waliendelea kuifunga Juventus kwa mikwaju ya penalti kwenye fainali iliyochezwa Old Trafford.

Milan pia walitinga kampeni za 2004-05 kama mabingwa wa Italia - Scudetto ya sita tangu Inter ilipotwaa ubingwa wa Serie A mnamo 1988-89.

Mmiliki Silvio Berlusconi alikuwa akijenga timu yake ya pili kubwa ya Milan na mfanyabiashara huyo aliyegeuka kuwa mwanasiasa alimwamini Carlo Ancelotti, mkufunzi wa timu iliyoshinda Vikombe vya Uropa mfululizo mnamo 1989 na 1990, kuwasilisha kipindi kingine cha mafanikio kama meneja.

Katika mechi ya robo fainali ya mkondo wa pili, mabeki wanne Cafu, Jaap Stam, Alessandro Nesta na Paolo Maldini walikaa nyuma ya Andrea Pirlo, Clarence Seedorf, Massimo Ambrosini na Kaka, huku Hernan Crespo - zamani wa Inter - na Andriy Shevchenko wakiwa mbele. Rui Costa alikuwa kwenye benchi.

Inter, wakati huo huo, walikuwa wametumia pesa nyingi kujaribu kushindana na Milan na Juventus. Mwenyekiti Massimo Moratti alivunja rekodi ya dunia ya uhamisho mara mbili ndani ya miaka mitatu, kwanza kumsajili Ronaldo kutoka Barcelona mwaka 1997 na kisha kumpata Christian Vieri kutoka Lazio mwaka 1999.

Crespo na Seedorf walikuwa wamefika Inter kwa mikataba mikubwa, lakini walishindwa kupata taji lolote muhimu, kabla ya kuungana kwenye mgawanyiko wa Milan.

Post a Comment

0 Comments