Baada ya Umoja wa Falme za Kiarabu (UAE) kutangaza kuwafungia visa raia wa Nigeria tangu Oktoba, 2022, Bodi ya Utalii ya Dubai imehamishia nguvu kwa nchi nyingine za Afrika kama Tanzania, Kenya, Afrika Kusini na Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo na kutambulisha mabalozi wanaowakilisha nchi hizo.
Miongoni mwa mabalozi hao, yumo msanii kutoka Afrika Kusini, Thabsie na msanii kutoka nchini Kenya Bahati ambapo bodi hiyo imeeleza kwamba inaendelea kutafuta mabalozi wa kuwakilisha nchi hizo katika kutalii Dubai.
Mabalozi hao wanategemewa kutumia umaarufu wao kuonesha watu wa nchi zao vitu ambavyo vinapatikana Dubai ili kuwavutia na wamejiunga na kampeni inayoitwa A to Z of Dubai inayoonesha watalii vitu vizuri vya Dubai.
Ripoti zinaeleza pia kwamba aliyekuwa Rais wa Nigeria Muhammad Buhari ameomba Dubai waondoshe kuwafungia kwa visa wanaijeria na kuonesha utayari wa kuzungumza juu ya tofauti zao na kuweza kuwakaribishia wanaijeria nchini humo tena.
0 Comments