Hivi karibuni wakati anahojiwa kwenye kipindi cha XXL cha Clouds FM, Diamond alitease ujio wa ngoma ambazo amewashikirisha wanamuziki heavyweight wa Marekani, Rick Ross na Rihanna.
Jumatano hii kupitia kipindi cha Campus Vibes cha Times FM, meneja wake, Sallam alifafanua zaidi kuhusu hatua iliyofikiwa ya collabo hizo. Sallam alidai kuwa collabo na Rick Ross imeshakalimika, huku ile ya Rihanna ikiwa kwenye hatua za mwisho kwakuwa tayari CV na historia ya Diamond imeshatumwa kwa uongozi wake kuweza kufikiwa maamuzi ya mwisho.
Kuhusu nyimbo alizoshirikishwa Diamond, Sallam alisema mwakwani itatoka ngoma aliyoshirikishwa na Burna Boy na Cassper Nyovest huku pia Dj Van wa Morocco akimshirikisha pamoja na msanii mkubwa wa Dubai.
Alidai kuwa kutokana na ubusy alionao hitmaker huyo wa Salome, imekuwa ngumu kupata muda wa kushoot video ya wimbo alioshirikishwa na msanii wa Jamaica, Alaine, wimbo alioshirikishwa na msanii wa Ivory Coast Serge Beynaud pamoja na kukamilisha wimbo anaoshirikishwa na rapper namba moja wa Cameroon, Stanley Enow.
Pia alidai kuwa Diamond atatumbuiza kwenye tuzo CAF 2016, Alhamis ya January 5, 2017 mjini Abuja, Nigeria na pia kwenye ufunguzi wa kombe la mataifa ya Africa (Total Africa Cup of Nations),itakayofanyika nchini Gabon kuanzia January 14.
0 Comments