Mtunzi: Enea Faidy
Ilipoishia sehemu ya Nne ( kama hukuisoma bofya hapa)
"hivi we demu unajisoma??" alisema Eddy kwa ukali. maneno hayo yalimshtua sana Dorice.
"Eddy! sijakuelewa!"
" unajisoma kweli? hivi kwanza unajua majamaa wanakucheka kwa sababu gani?" maneno ya Eddy yalimfanya Dorice .....
SEHEMU YA 5
...DORICE alimtazama Eddy kwa mshangao wa hali ya juu kwani tangu walipoanza mahusiano hakuwahi kumuona akiwa na chuki dhidi yake kwa kiasi kile. Dorice alikosa ujasiri wa kuzungumza chochote kwa wakati ule kwani alihisi viungo vyake vyote vinakosa nguvu. Akabaki ameduwaa kama zuzu mbele ya Eddy.
"we Dorice nimekuuliza unajua wanakucheka nini darasani?" aliuliza Eddy kwa ukali.
"Sijui" alijibu Dorice kwa huzuni
" Sasa kama hujui wanakucheka jinsi ulivyomchafu, hebu jiangalie hizo kamasi ulizojipaka kama mtoto asiyejua hata kutembea, pili hiyo yako chafu, na tatu...." kabla Eddy hajamaliza Dorice alishtuka sana kusikia vile kwani alipofika darasani asubuhi alikuwa msafi kama ilivyokuwa kawaida yake.
"Eddy umesemaje?!" aliuliza Dorice kwa mshangao. Na wakati huo Doreen alikuwa alikuwa amejificha nyuma ya darasa karibu na waliposimama akina Dorice, na aliweza kusikia kila kitu kinachozungumzwa. Alisikiliza kwa umakini sana huku akiyafurahia majibu ya Eddy Kwa Dorice.
" Hujanisikia? tena ukome kunifuatilia, usahau kama nilishakuwa mpenzi wako , unifute akilini mwako, sikupendi?" alisema Eddy akiwa amenuna kama aliyekula ndimu.
"unasemaje Eddy! hebu rudia nisikie"
"Sikutaki , sikupendi na sikuhitaji!" alisema Eddy huku akiondoka
"Eddy! Eddy! nimekukosea nini mpenzi wangu?"
"Achana na Mimi Dorice! huna hadhi ya kuwa na mimi , demu mwenyewe huna hata mvuto!" alisema Eddy na kusonya. Kisha akaenda zake darasani.
Alimwacha Dorice kwenye bahari ya simanzi na machozi yasiyoweza kuzuilika. Alilia kwa uchungu kama MTU aliyefiwa na MTU muhimu, lakini kilio hicho cha Dorice kilikuwa shangwe na furaha kwa Doreen. Alijiona kama mshindi kwa kufanikiwa kulivuruga penzi la Eddy na Dorice bila hata huruma kwani wawili hao walipendana sana na walikuwa na malengo makubwa katika maisha ikiwa ni pamoja na kufunga ndoa pindi watakapotimiza malengo yao.
Doreen alicheka kwa dharau kisha akaondoka zake na kwenda darasani, ambapo alimfuata Eddy pale alipokuwa amekaa.
Eddy alimkaribisha Doreen kwa tabasamu mwanana na macho ya matamanio.
==> Endelea Nayo <
0 Comments