SHINYANGA! Mama mmoja mkazi wa Kahama mkoani Shinyanga aliyejitambulisha kwa jina la Mwajei amedai kutelekezwa na mumewe (jina tunalihifadhi kwa sasa) kisa ‘buku’ tatu (3000) ya matibabu ya mtoto wao ambaye aligongwa na pikipiki.
Akizungumza kwa uchungu Mwajei alisema kuwa tukio hilo lilitokea Juni 7 mwaka huu baada ya mtoto wao kugongwa na pikipiki kisha kulazwa katika Hospitali ya Wilaya ya Kahama ambapo kila alipomtafuta mumewe kwa ajili ya kumpa pesa ya matibabu hakueleweka.
“Mtoto aligongwa na pikipiki nikampeleka hospitali lakini kila nikimpigia mume wangu na kumuomba Sh. 3000 ya matibabu anasema kuwa kasafiri yuko Dodoma, mara yuko Singida, nateseka na huyu mtoto jamani,” alisema mama huyo.
Alipotafutwa mume wa Mwajei kwa njia ya simu, iliita bila kupokelewa na hata alipotumiwa ujumbe mfupi wa maneno hakujibu lolote
0 Comments