Mvutano mkali umeibuka bungeni, mjini Dodoma leo wakati wabunge wa ya upinzani wakichangia mjadala wa bajeti mbili za Ofisi ya Rais-Tamisemi na Utawala Bora baada ya kudai kuwa serikali inaongozwa bila kuzingatia utawala bora.
Wabunge hao wamepinga hatua ya serikali kusitisha urushaji wa matangazo ya Bunge moja kwa moja kutokea Dodoma.
Wakiongozwa na mbunge wa Iringa Mjini (Chadema), Mchungaji Peter Msigwa, wabunge hao walikuwa wakipokezana kuishambulia serikali katika maeneo hayo mawili jambo lililozua mvutano mkali kati yao na Naibu Spika, Dk Tulia Ackson na Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo, Nape Nnauye ambaye alizomewa mara aliposimama kutoa ufafanuzi wa kusitisha matangazo ya Bunge.
Hata hivyo, Naibu Spika Dk Ackson alimuita mbunge wa Kilwa Kusini (CUF), Selemani Said Bungara kuwa ni bwege.
“We mheshimiwa bwege hebu acha kuonyesha ubwege wako. Alitoa kauli hiyo wakati mbunge huyo aliposimama kupingana na maelezo na Nape bila kufuata kanuni za chombo hicho cha kutunga sheria.
Bungara jina lake la utani ni bwege na mara nyingi amekuwa akitaka watu wamuite hivyo.
0 Comments