Akiongea kwenye mahojiano na gazeti la Champion, Sallam alisema: Sina tatizo kabisa, akitaka tufanye kazi nitamweleza mahitaji yangu akikubali tutafanya kazi. Nilishawahi kukutana na Kiba, Nairobi, alinifuata akaomba tupige picha, sikuwa na kinyongo, tukapiga ikawa safi japokuwa ile picha aliitumia kunitukanisha baadaye.
Akifafanua kuhusu hilo, Sallam alisema: Hakuiweka yeye katika mtandao, aliitoa kwa mashabiki wake ambao wakasema nimeenda Nairobi kumfuata Ne-Yo halafu nikafukuzwa, wakasema mimi ndiyo niliomba kupiga picha na Kiba, ikawa gumzo sehemu nyingi. Ukweli nilikuwa na Ne-Yo na Diamond ambaye alikwenda pale kurekodi, yeye Kiba alikuwa Coke Studio.
Anasema Kiba alimuomba radhi na kudai kuwa aliwatumia wapost lakini wakaweka maneno yao.
KUHUSU ANAVYOMCHUKULIA ALIKIBA KIMUZIKI
Siwezi kusema anakosea wapi, maana kila msanii ana njia zake. Wimbo wake wa Mwana ni mkali na ulifanya vizuri yawezekana anakosea kwenye ‘market’. Kuna vitu lazima ulazimishe, hata Diamond yupo juu lakini hawezi kutoa kitu halafu akatulia tu akaacha watu wapende wenyewe. Kila mtu ana staili yake yawezekana yeye hataki kwenda kwenye staili kama hiyo, ndiyo maana kuna muda huwa nasema huwezi kumfananisha Diamond na Ali kwa sababu wanaimba muziki wa tofauti. Wote ni Bongo Fleva lakini staili zao ni tofauti, kwa mtu anayefuatilia muziki anaweza kugundua hilo.
KUHUSU BIFU YA DIAMOND NA ALIKIBA
Hakuna bifu kabisa, mimi nafahamu hilo. Wameshakutana na kusalimiana na hakuna chochote. Nasema kabisa wanapiga stori na wanaongea ‘fresh’ kabisa. Kinachotokea ni kwamba watu wanawauliza kama wana bifu kwa hiyo wenyewe wanasema hawana bifu basi, lakini kwa kuwa hakuna maelezo mengi watu wanachukulia hivyo.
Kuhusu madai kuwa uongozi wa Diamond unafanya fitna ya kuzuia video za Kiba zisipigwe katika vituo vikubwa vya nje kama MTV na Trace, Sallam alisema:
Siyo kweli. Kiba na ana nguvu kubwa MTV na Trace kuliko Diamond kwa ajili ya Seven (ni mmoja wa wasimamizi wa Ali Kiba). Seven alikuwa mfanyakazi wa MTV, anawajua watu wote wa MTV, hata yule bosi wa Trace wa sasa alikuwa chini ya Seven, ndiyo maana hata video yake ya Chekecha Cheketua ilichezwa wiki nzima mfululizo ikiwa ni ‘Exclusive’.
Wenzetu katika vituo wanaangalia vigezo vyao. Nikupe siri kuwa wakati naanza kazi na Diamond, alikuwa anabaniwa kweli zisipigwe kabisa hata Channel O.
Aliendelea: Siwezi kutaja jina lakini nyimbo zilikuwa zinapelekwa DStv hapo lakini anaambiwa hazina viwango, zinarudi. Aliyekuwa anafanya hivi ni Mtanzania na ni mhusika mkubwa wa muziki wa Tanzania. Nilimfuata nikamchana ‘live’ baadaye tukaamua kazi zetu kuzipitishia Nigeria kisha tukarudi hapa na kila kitu kikawa rahisi. Niwashauri watu kuwa wafanye kazi na watangaze kazi zao dunia ya sasa hakuna kitu kinachoenda chenyewe tu.
0 Comments