SIMBA inatia huruma. Hiyo ni baada ya kufungwa bao 1-0 na Toto Africans ya Mwanza katika mchezo wa Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara jioni ya leo Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Kiboko ya Simba leo alikuwa ni kiungo Waziri Junior aliyefunga bao hilo pekee dakika ya
20 kwa shuti kali la umbali wa mita 20 lililomshinda kipa Muivory Coast, Vincent Angban.
Matokeo hayo yanaifanya Simba ishindwe kuwaondoa kileleni mabingwa watetezi, Yanga SC waliorejea juu jana baada ya ushindi wa 1-0 dhidi ya Mtibwa Sugar.
Simba inayobaki na pointi zake 57 baada ya kucheza mechi 25, inaendelea kuwa nafasi ya pili, mbele ya Azam FC yenye pointi 55 za meci 24, wakati Yanga wenye pointi 59 za mechi 24 wapo juu.
Kikosi cha Simba SC kilikuwa; Vincent Angban, Hassan Kessy, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, Novat Lufunga, Hassan Isihaka, Jonas Mkude, Peter Mwalyanzi, Awadh Juma, Daniel Lyanga, Hamisi Kiiza na Mussa Mgosi
Toto Africans; Mussa Kirungi, Erick Mlilo, Salum Chukwu, Yusuph Mlipili, Hassan Khatib, Carlos Protas, Jama Soud, Abdallah Seseme, Waziri Junior, Edward Christopher na Jafari Mohammed.
0 Comments