Header Ads Widget

Bomba la Mafuta kutoka Uganda hadi Tanga kukamilika 2020


WAZIRI wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo amesema kuwa bomba la mafuta kutoka Uganda hadi Tanga litakuwa limekamilka kufikia 2020 hivyo kilichobaki ni kuanza utekelezaji wa kuanza kujenga bomba hilo.

Profesa Muhongo ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam wakati alipokutana na waandishi wa habari juu ya mikakati walioweka katika kutekeleza ujenzi wa bomba hilo, amesema kuwa wataalam katika sekta mbalimbali kutoka Uganda na Tanzania wamekutana leo jijini Dar es Salaam kuweza kuweka mikakati hiyo ya kuanza kutekeleza bomba hilo.

Muhongo amesema kuwa kutokana na maagizo ya Rais Dk.John Pombe Magufuli na Rais wa Uganda, Yoweri Kaguta Mseveni ya mradi wa bomba la mafuta watendaji kazi yao ni kuanza kufanya utekelezaji na wataweza kumaliza kabla ya mwaka huo baada ya kupata muongozo wa wataalam wataowasilisha Mei 26 Oima nchini Uganda.



Waziri wa Nishati na Madini, Profesa Sospeter Muhongo (katikati) akielezea uzoefu wa Tanzania kwenye ujenzi wa miradi ya mabomba ya gesi na mafuta katika mkutano huo. Kushoto ni Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni na kulia ni Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini, Profesa Justin Ntalikwa.

Waziri huyo amesema kuwa Uganda imetoa asilimia 40 kwa nchi Jumuiya ya Afrika Mashariki kuweza kununua hisa hizo ili kuwa na sehemu ya kunufaika na bomba hilo ikiwa hisa hizo zinauzwa kwa Dola za Kimarekani Bilioni 4.7.

Amesema kuwa kwa nchi makini haiwezi kuacha kununua hisa hizo kutokana na faida ya mradi huo na nchi itakayoacha kununua hisa hizo sio makini.

Amesema bomba hilo lina umuhimu kwa kujengwa nchini ambapo Tanzania itaweza katika kujenga bomba la gesi kwenda uganda kutokana na uhitaji wa Waganda wa gesi inayozalishwa nchini.




Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia madini Profesa James Mdoe ( wa kwanza kushoto, waliokaa mbele); Naibu Katibu Mkuu wa Wizara ya Nishati na Madini anayeshughulikia nishati Dk. Mhandisi Juliana Pallangyo ( wa pili kushoto waliokaa mbele) pamoja na wataalam wengine wa Wizara ya Nishati na Madini wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Maendeleo ya Madini Nchini Uganda, Mhandisi Irene Muloni (hayupo pichani) katika mkutano kati ya nchi ya Tanzania na Uganda lengo likiwa ni kujadili mpango wa ujenzi wa bomba la mafuta kutoka Hoima, Uganda hadi katika bandari ya Tanga nchini Tanzania.
 
mpekuzi blog

Post a Comment

0 Comments