Header Ads Widget

TANZANIA: WIZARA YA UJENZI YAPIGA MARUFUKU "KUCHATI" SAA ZA KAZI


Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano nchini Tanzania imewapiga marufuku wafanyakazi wake ''Kuchati'' katika mitandao ya kijamii kwa kutumia simu katika muda wa saa za kazi.



Waziri wa Wizara hiyo Makame Mbarawa amekemea tabia ya baadhi ya wafanyakazi, kutumia muda mwingi maofisini kuperuzi katika mitandao ya kijamii pamoja na kupiga porojo, hali inayosababisha kushuka kwa uzalishaji na maendeleo.

Ameongeza kuwa watakaobainika kufanya hivyo watachukuliwa hatua za kisheria bila ya kuonewa haya, na pia kuwataka wafanyakazi wa wizara yake kuwa na bidii ya kazi na weledi.

Lakini hata hivyo, marufuku hiyo itaweza kufanikiwa?, kutokana na ukubwa wa matumizi ya mtandao, huku walengwa wakiona wananufaika nayo.

Kutokana na kukua kwa teknolojia ya habari na mawasiliano duniani, watu wengi hususan vijana wamekuwa wakitumia muda mwingi katika mitandao ya kijamii, kupitia simu za mikononi na kompyuta, kwa lengo la kupata taarifa mbalimbali za ulimwengu na pia kujifunza.

Nchini Tanzania matumizi ya huduma ya mawasiliano imekuwa kwa kasi katika siku za hivi karibuni, hususan kupitia mitandao ya WhatsApp, Facebook, Twitter na blogi mbalimbali.

Post a Comment

0 Comments