Header Ads Widget

TAZAMA PICHA ZA MAPOKEZI YA MBWANA SAMATTA (@SAMAGOALS) UWANJA WA NDEGE DAR



Waandishi maarufu wa habari za michezo Tanzania, Tullo Chambo (kushoto) na Ramadhani Mkandemba (kulia) wa gazeti la Tanzania Daima wakiwa na Mwanasoka Bora Anayecheza Afrika, Mbwana Ally Samatta (katikati) baada ya kuwasili Alfajiri ya leo Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere, Dar es Salaam kufatia kushinda tuzo hiyo ya Shirikisho la Soka Afrika (CAF) usiku wa juzi mjini Abuja, Nigeria


Wapenzi na mashabiki maarufu wa soka nchini, Esther na Bob Chicharito (kulia) walijitokeza pia kumlaki Samatta. Mshambuliaji huyo wa TP Mazembe ya DRC alipata mapokezi mazuri licha ya kuwasili usiku wa manane

Wapenzi mbalimbali wa soka wakimkabidhi zawadi Mbwana Samatta Uwanja wa Ndege wa JNIA

Kutoka kulia ni Meneja wa Samatta, Jamal Kisongo, Samatta mwenyewe na mchezaji mwenzake wa Tanzania na TP Mazembe, Thomas Ulimwengu

 
Mwandishi maarufu wa habari za michezo, Mwani Nyangassa naye alijitokeza akiwa na fulana maalum ya "Hongera Samatta'

Post a Comment

0 Comments