Header Ads Widget

Ronaldo anatajwa kutumia zaidi ya milioni 400 za kibongo kujipoza machungu ya kukosa Ballon d’Or ….




Mshambuliaji wa kimataifa wa Ureno anayekipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Cristiano Ronaldo, January 11 mjini Zurich Uswiss alishuhudia mshambuliaji wa kimataifa wa Argentina na klabu ya FC Barcelona Lionel Messi ambaye pia ni mpinzani wake mkubwa akitwaa tuzo ya tano ya Ballon d’Or akiwashinda Neymar na Ronaldo.


Lionel Messi na Carli Lloyd wa USA waliotangazwa washindi wa tuzo za wachezaji bora wa Dunia kwa upande wa wanawake na wanaume

Siku moja baada ya Ronaldo kukosa kutwaa tuzo ya nne ya Ballon d’Or na kumuona Lionel Messi akitwaa ya tano, Ronaldo ameonekana na gari jipya la kifahari, ambapo inatajwa kuwa huenda kanunua ili kujipoza machungu ya kukosa tuzo ya nne ya Ballon d’Or.


Ronaldo akiwa na gari lake jipya aina ya Porsche 911 Turbo S

Ronaldo kanunua gari aina ya Porsche 911 Turbo S lenye thamani ya pound 146000 ambazo ni zaidi ya milioni 400 za kibongo, Ronaldo amewahi kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Dunia mara tatu, wakati mpinazani wake mkubwa Lionel Messi usiku wa January 11 alitwaa tuzo yake ya tano ya Ballon d’Or Zurich Uswiss.

Post a Comment

0 Comments